Watanzania na Wanasimba wote wameaswa kufurika kwa wingi Uwanja wa Taifa kesho kuishangilia Simba itakapokuwa ikiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya awali.
Simba itachuana na Mbabane Swallows kutoka Uswatini katika mchezo unatarajiwa kuanza saa kumi jioni.
Ni mchezo ambao Simba inahitaji kuibuka na ushindi mnono ili kuwa katika nafasi nzuri ya kutinga raundi ya kwanza ya michuano hiyo
Mchezo wa marudiano baina ya timu hizo utapigwa huko Uswatini (zamani Swaziland) wiki ijayo.