Uongozi wa klabu ya Yanga uko mbioni kumalizana na Lipuli Fc ili kukamilisha usajili wa nahodha wa timu hiyo ambaye ni mlinzi anayemudu nafasi za beki wa kati na pembeni, Ally Sonso.
Sonso amekuwa katika kiwango bora msimu huu akiwa miongoni mwa wachezaji walioitwa na Emmanuel Amunike kuunda kikosi cha timu ya Taifa mwezi uliopita.
Sonso amethiboitisha kumalizana na Yanga akiwa tayari kuelekea Jangwani lakini akisubiri viongozi wa Lipuli Fc wamalizane na wenzao wa Yanga.
Sonso anakuwa mchezaji wa pili kuwaniwa na Yanga katika kipindi cha miezi sita baada ya mabingwa hao wa kihistoiria kumkosa Adam Salamba aliyetua Simba mwishoni mwa msimu uliopita.