Mrisho Ngasa ni kama amezaliwa upyaaaa kwani mambo anayofanya dimbani sio ya kawaida. Leo amefunga bao lake la nne msimu huu akitupia katika michezo miwili mfululizo.
Anachokifanya Ngasa sasa ni kuwapa majibu ‘mbashara’ wale wote waliokuwa wanam-beza na kusema umri umemtupa mkono.
Amekuwa na ushirikiano mzuri sana na Heritier Makambo ambaye kasi yake ya kupachika mabao tayari imeanza kuwatia hofu upande wa pili
Amefikisha mabao saba na inaonekana atafunga sana msimu huu.
Makambo ni mshambuliaji aliyekamilika, amedhihirisha hilo na anao uwezo wa kufunga aina zote za mabao.
Kwa hakika kikosi cha Yanga sasa kimeiva.
Licha ya changamoto za nje ya uwanja, wachezaji wa Yanga wamekuwa wakicheza kwa kujituma, Na sasa kuna kitu kingine kimeongezeka, WANAJIAMINI
Ile burudani ya ‘kampa-kampatena’ imeanza kurejea. Sasa Yanga inapata ushindi huku pia ikicheza mpira ‘mwingi’ tofauti na ilivyokuwa mwanzoni mwa msimu
Yanga hii itawashangaza wengi msimu huu..