SAKATA La Beno KAKOLANYA

Mlinda lango Beno Kakolanya hakusafiri na kikosi cha Yanga mkoani Mbeya ikielezwa ana matatizo ya kifamilia.

Hata hivyo taarifa nyingine zinadai kuwa Kakolanya amegoma kucheza na anataka kuvunja mkataba wake akiidai klabu hiyo malimbikizo ya mishahara ya miezi mitano

Wengi wamekuwa wakijiuliza ni kweli Yanga imeshindwa kumlipa mchezaji huyo hadi kufikia hatua ya kutaka kuvunja mkataba wake?

Hivi karibuni kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera alitoa ushauri kwa viongozi wa timu hiyo kuwa ni vyema wakamalizana na wachezaji wenye madai kuliko kusajili wachezaji wapya ambao hakuna uhakika wa kulipa mishahara.

Taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii leo zinadai Kakolanya tayari amevunja mkataba wake na sasa ni mchezaji huru.

Simba inahusishwa kutaka kumsajili mlinda lango huyo aliyeonyesha ubora wa hali ya juu msimu huu.

Viongozi wa Yanga watakuwa na majibu sahihi juu kinachoendelea kumuhusu mlinda lango Beno Kakolanya.