
Nyoni amepona, huyu ndio ‘Waziri wa Ulinzi’ Simba
Baada ya kuwa nje tangu mwezi Januari, Nyoni alirejea kikosini jana kuwakabili Vita Club na hakika alidhihirisha kwa nini mashabiki walihitaji sana urejeo wake
Licha ya kutocheza kwa muda mrefu Nyoni hakuonyesha dalili yoyote ya kutokuwa ‘fit’ akiwadhibiti ipasavyo washambuliaji wa Vita walio-ongozwa na Makusu
Nyoni alifanya kazi ya ziada kwenye safu ya ulinzi ya Simba akiwa kiongozi aliyesaidia kuwapanga wenzake katika kuhakikisha wapinzani hawalifikii lango
Juzi kocha Mkuu wa Taifa Stars Emmanuel Amunike alimrejesha katika kikosi cha timu ya Taifa kuchukua nafasi ya Andrew Vicent wa Yanga
Unapozungumzia ushindi wa mabao 2-1 iliyopata Simba dhidi ya Vita Club jana, unazungumzia juhudi na kujituma kwa wachezaji wa Simba, Nyoni akiwa mmoja wa wachezaji waliocheza vizuri sana