Simba ilivyoizidi ujanja AS Vita kwa Tuyisenge

Uongozi wa klabu ya Simba tayari umemalizana na mshambuliaji wa Gor Mahia Jacques Tuyisenge ambaye pia alikuwa akiwaniwa na AS Vita Club ya DR Congo

Baada ya kumpoteza mshambuliaji wake Jean Mark Makusu aliyetimkia nchini Morocco, Vita ilikuwa mbioni kumsajili Tuyisenge kuchukua nafasi yake

Hata hivyo Meddie Kagere aliyekuwa ‘pacha’ wa Tuyisenge katika klabu ya Gor Mahia ambaye pia ni pacha wake katika kikosi cha timu ya Taifa ya Rwanda, amechangia kwa kiasi kikubwa kumshawishi Tuyisenge kutua Simba

Simba imempa Tuyisenge mkataba wa awali wa miaka miwili akitarajiwa kuanza kazi mwishoni mwa msimu

Tuyisenge alikutana na mabosi wa Simba juzi usiku katika kikao ambacho kilikuwa na mafanikio kwa pande zote mbili kufikia makubaliano