Simba kucheza mechi saba kwa wiki mbili ligi kuu

KeshoJumatano Simba inarejea rasmi kwenye mchakamchaka wa ligi kuu ya Tanzania Bara kwa kuikabili Coastal Union katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga

Kutokana na muda mchache uliobaki kabla ya ligi hiyo kumalizika mwezi ujao, Simba inakabiliwa na ratiba ya kucheza mfululizo ambapo katika kipindi cha wiki mbili itashuka dimbani mara saba

Baada ya mchezo dhidi ya Coastal Union April 17, mchezo utakaofuata ni dhidi ya Kagera Sugar utakaopigwa mkoani Kagera katika uwanja wa Kaitaba April 20

April 23 Simba itakuwa Mwanza kuchuana na Alliance Fc katika mchezo utakaopigwa uwanja wa CCM Kirumba kisha kurudi dimbani hapo April 26 kumenyana na KMC

Siku mbili baadae April 28 Simba itaelekea mkoani Mara kuikabili Biashara United kabla ya kuelekea mkoani Mbeya ambako May 01 itacheza na Tanzania Prisons kwenye uwanja wa Sokoine kisha kurejea tena dimbani hapo May 03 kuumana na Mbeya City