Aussems ataja kilichoiponza Simba mchezo dhidi ya Kagera Sugar

Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema timu yake haikucheza vizuri kwenye kipindi cha kwanza katika mchezo dhidi ya Kagera Sugar ambao Simba ilipoteza kwa mara ya pili msimu huu kwa kufungwa mabao 2-1

“Nawapongeza Kagera Sugar kwa sababu walikuwa na mchezo mzuri katika kipindi cha kwanza, sisi hatukuwa bora,” alizungumza Aussems baada ya mchezo jana

“Walitumia udhaifu wetu kuweza kufunga mabao mawili ambayo kwetu haikuwa rahisi kuyarejesha yote kwenye kipindi cha pili licha ya kurekebisha makosa tuliyofanya kwenye kipindi cha kwanza”

“Wachezaji wangu walicheza dakika 45 za kipindi cha pili na kufanikiwa kufunga bao moja na kutengeneza nafasi nyingine ambao tulishindwa kuzitumia. Hata hivyo mchezo ni dakika 90”

Baada ya mapumziko ya Pasaka, Simba itaelekea mkoani Mwanza kuikabili Alliance Fc kwenye mchezo mwingine wa ligi utakaopigwa keshokutwa April 23 katika dimba la CCM Kirumba