Penati hazina mwenyewe, tuwavumilie wachezaji wanapokosa

Katika mchezo wa kwanza wa ligi ya mabingwa dhidi ya TP Mazembe, nahodha John Bocco alikosa mkwaju wa penati tukio ambalo lilimfanya ashushiwe lawama nyingi na mashabiki

Hata hivyo leo katika mchezo dhidi ya KMC, Bocco ameifungia Simba mkwaju muhimu wa penati ulioipandisha Simba hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1

Hata hivyo katika mchezo huo Meddie Kagere alikosa penati ya kwanza iliyotolewa na mwamuzi

Matukio haya yanadhihirisha kuwa hakuna sababu ya kuwalaumu wachezaji pale wanapokosa mikwaju ya penati kwani hakuna mchezaji mwenye uhakika wa kufunga penati kwa asilimia 100

Katika kikosi cha Simba Bocco ndiye mwenye rekodi nzuri ya kufunga mikwaju ya penati.

Kwenye ligi Bocco amefunga mikwaju yote mitano aliyopiga msimu huu