FT : Biashara United 0-2 Simba

Simba imeendeleza umwamba wake kwenye ligi kuu ya Tanzania Bara baada ya leo kuifumua Biashara United mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Karume, Mara

Simba imefikisha alama 69 sasa ikitofautiana na Yanga kwa tofauti ya alama tano tu huku kibindoni ikiwa na michezo mitano ya viporo

Shukrani za kipekee zimwendee nahodha John Bocco aliyefunga mabao yote mawili kwenye kipindi cha kwanza na kuihakikishia Simba alama tatu muhimu

Bocco amefikisha mabao 14 akichupa mpaka nafasi ya tatu kwenye orodha ya vinara wa mabao nyuma ya Makambo mwenye mabao 15

Aidha Bocco amefikisha idadi ya mabao aliyofunga msimu uiliopita

Katika mchezo huo Simba ilipata pigo baada ya kiungo wake Haruna Niyonzima kutolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kumtolea maneno machafu mwamuzi

Simba imemaliza michezo ya kanda ya ziwa na sasa inarejea jijini Dar es salaam ambapo Jumanne itachuana na JKT Tanzania, mchezo utakaopigwa uwanja wa Uhuru