
Lakini asikwambie mtu, mzuka wa mashabiki wa timu hiyo mkoani Mbeya, unawafanya mabingwa hao wa Tanzania Bara kutojihisi kabisa kama wako ugenini
Katika mchezo dhidi ya Mbeya City ambao Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-1, mashabiki wa ‘Mnyama’ walifunika dimba la Sokoine.


Leo tena wameahidi kuwa sambamba na timu yao kuhakikisha alama zote tatu zinakwenda Msimbazi
Mchezo unatarajiwa kuanza saa kumi kamili jioni na tayari mashabiki wameanza kujisogeza uwanja wa Sokoine