Simba yasaka alama nyingine tatu Mbeya

Baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mbeya City juzi, leo Simba inarejea tena uwanja wa Sokoine kuikabili Tanzania Prisons

Mchezo ambayo kama Simba itaibuka na ushindi, itasogea zaidi kileleni mwa msimamo wa kwani itabakisha alama mbili tu kuifikia Yanga

Meneja wa Simba Patrick Rweyemamu amesema wachezaji wa timu yake wako katika hali nzuri, wamejiandaa vyema kuweza kupata alama nyingine tatu leo

Tanzania Prisons ilitua mkoani Mbeya juzi ikitokea Dar es salaam ambako ilifungwa na Yanga mabao 2-1

Kocha Mkuu wa timu hiyo Adolph Richard amesema wanatarajia mchezo hautakuwa mwepesi lakini wamepania kupata matokeo ili kujiweka salama na hatari ya kuteremka daraja

Baada ya mchezo huo Simba itarejea jijini Dar es salaam ambako itakuwa na nafasi ya kutwaa ubingwa katika michezo sita itakayocheza uwanja wa Taifa/Uhuru