Ligi Kuu ya Tanzania Bara inaendelea leo ambapo mabingwa watetezi Simba watashuka katika uwanja wa Uhuru kuikabili Azam Fc katika mchezo usiotabirika
Huo ni mchezo wa duru ya pili msimu huu Simba ikishinda mchezo wa kwanza kwa mabao 3-1
Huo ni mchezo wa duru ya pili msimu huu Simba ikishinda mchezo wa kwanza kwa mabao 3-1
Simba inayowania ubingwa wa pili mfululizo, kama itaibuka na ushindi leo basi itabakisha alama sita tu ili iweze kutetea ubingwa wake
Azam Fc inayoshika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi, haina matumaini ya kutwaa ubingwa wala kumaliza kwenye nafasi ya pili
Hata hivyo kocha Msaidizi wa timu hiyo Iddi Cheche amesema baada ya kufungwa katika mchezo wa kwanza, hawatakubali kupoteza mchezo dhidi ya Simba kwa mara ya pili
Mkufunzi wa Simba Patrick Aussems amesema Azam Fc ni timu nzuri lakini hawaihofii na baada ya kupoteza mchezo uliopita, wanahitaji kushinda leo
Mchezo huo unatarajiwa kuanza saa kumi jioni