SEVILLA – Kuwasili Dar Mei 21

Leo Jumamosi Sevilla inakamilisha mchezo wa mwisho ligi kuu ya Hispania , La Liga kwa kucheza na Athletic Club

Kama itashinda mchezo huo, Sevilla inayoshika nafasi ya sita kwenye msimamo wa La Liga , inaweza kukata tiketi ya kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa msimu ujao

Baada ya mchezo huo, kikosi cha Sevilla itaanza safari ya kuja nchini tayari kwa mchezo wa Kimataifa wa kirafiki dhidi ya mabingwa wa Tanzania Bara, Simba

Sevilla inatarajiwa kuwasili nchini Mei 21 kuelekea mchezo huo utakaopigwa Mei 23, uwanja wa Taifa kuanzia saa moja jioni

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, (TFF) limesema kuwa ujio wa timu ya Sevilla kutoka nchini Hispania chini ya SportPesa Tanzania utaongeza hamasa na maendeleo ya mpira wa miguu nchini.

TFF imewataka wachezaji wa Simba kutumia fursa ya mechi hiyo kuonyesha uwezo na vipaji vyao ili kujitangaza

Rais wa TFF, Wallace Karia amesema kuwa Sevilla FC ni timu kubwa yenye historia kubwa katika soka duniani na hivyo ujio wao utawavutia mashabiki wa soka hata wa nchi jirani ili kuja kushuhudia wachezaji nyota wa wanaocheza bara la Ulaya.

Leave a comment