CHIRWA: Aiwekea Ngumu Azam Arudi au Asirudi?

Mshambuliaji wa Azam Fc Obrey Chirwa amegoma kusaini mkataba mpya kunako klabu hiyo mpaka mwishoni mwa msimu

Azam Fc imekuja na utaratibu tofauti wa kuwaongezea mikataba wachezaji wake kabla ya mikataba yao ya awali kumalizika

Timu hiyo tayari imewapa mikataba wachezaji wake waandamizi isipokuwa Chirwa aliyejiunga na timu hiyo kwa mkataba wa miezi sita wakati wa dirisha dogo la usajili

Hivi karibuni kocha Mwinyi Zahera alieleza kuvutiwa na kiwango cha mshambuliaji huyo raia wa Zambia

Zahera alisema Chirwa ni bonge la mchezaji, lakini alikataa kuweka wazi kama anaweza kumrejesha tena kikosini kwa ajili ya msimu ujao

Alitaja hali ngumu ya kiuchumi Yanga ilikuwa sababu ya yeye kukataa asisajiliwe aliporejea kutoka Misri mwishoni mwa mwaka jana

“Chirwa ni mchezaji mkubwa na anapambana sana katika uchezaji wake hata kwa mechi nilizomuona ana kitu ambacho wengine hawana, ila nilimkataa kwa kuwa hawezi kuvumilia matatizo,” alisema

Leave a comment