KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, imeingia udhamini na Kampuni ya GF Truck and Equipment kwa ajili ya mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) dhidi ya Lipuli Juni Mosi mwaka huu.
Mchezo huo umepangwa kufanyika Uwanja wa Ilulu, Lindi.
Zoezi la kuingia mkataba baina ya pande hizo mbili limefanyika kwenye ofisi za GF Truck, iliyowakilishwa na Mkurugenzi wake, Imran Karmali, huku Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin ‘Popat’, akiiwakilisha timu hiyo.
GF Truck ni moja ya kampuni bora, inayojihusisha na uzaaji wa magari ya FAW na mitambo ya ujenzi na uchimbaji ya XCMG, ikiwa imewekeza vilivyo kwenye sekta ya michezo.


A

zam FC imejipanga vilivyo kuelekea mchezo huo wa fainali, ikiwa imejiwekea malengo ya kutwaa taji na kukata tiketi ya kushiriki Kombe la Shirikisho Afrika msimu ujao.