MO DEWJI APONGEZA UBINGWA SIMBA

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba Mohammed Dewji ‘Mo’ ameipongeza timu hiyo kwa kufanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Tanzania Bara kwa msimu wa pili mfululizo

Mo amesema mafanikio hayo yamepatikana kutokana na juhudi zilizofanywa na wachezaji, benchi la ufundi, viongozi na wadau wote wa klabu ya Simba kila mmoja kwa nafasi yake

“Mungu mkubwa. Pongezi kwa wachezaji, benchi la ufundi, viongozi, wanachama, mashabiki, na wapenzi wote wa SIMBA, tumeshinda! Najivunia mafanikio haya,” amesema Mo

Naye Msemaji wa Simba Haji Manara amewapa shukrani za kipekee wachezaji, benchi la ufundi pamoja na mashabiki wa timu hiyo kwani wamekuwa na mchango mkubwa kwa mafanikio ya Simba msimu huu

“Tumshukuru Mungu muweza aliyetaka Simba iwe Bingwa tena”

“Tuwapongeze sana Wachezaji wetu wote, Benchi la ufundi chini ya kocha Patrick Aissems, lakini kipekee tuwashukuru nyie Wanachama na Washabiki wetu ambao mimi nnaamini ndio chachu ya huu ubingwa”

“Kwangu shujaa wa kwanza Simba ni Mshabiki wetu, Tunawashukuru sana”

Simba imetwaa ubingwa leo baada ya kuifunga Singida United mabao 2-0

Mabao ya Meddie Kagere na John Bocco yalitosha kuihakikishia Simba ubingwa baada ya kufikisha alama 91 kwenye msimamo wa ligi

Alama hizo haziwezi kufikiwa na timu nyingine yoyote katika michezo iliyobaki

Simba imeibuka na ubingwa huku ikiwa na michezo miwili mkononi

Leave a comment