Simba imefanikiwa kutetea ubingwa kwa msimu wa pili mfululizo baada ya leo kuichapa Singida United mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Namfua
Mabao ya Meddie Kagere na John Bocco yalitosha kuihakikishia Simba ubingwa wake wa 20
Simba imefikisha alama 91 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine hata kama zitashinda michezo yote iliyobaki

Wachezaji, benchi la Ufundi na viongozi wa Simba wanastahili pongezi kwa mafanikio haya ya kikosi cha Simba
Ubora wa timu, ushirikiano baina ya Wana Msimbazi ndio sababu kubwa iliyopelekea kuibuka na ubingwa wa pili mfululizo
Msimu haukuwa mwepesi kutokana na Simba kushiriki katika mashindano mengi, lakini juhudi za wachezaji zimewezesha kupatikana kwa mafanikio haya
Simba imejihakikishia tiketi ya kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa msimu ujao, mashindano ambayo tayari imepata uzoefu mkubwa msimu baada ya kufika hatua ya robo fainali
Hongera Wachezaji, Hongera Benchi la Ufundi, Hongera Viongozi, Hongera Mashabiki wa Simba……!