TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA LEO IJUMAA

Liverpool, Manchester United na Arsenal wanataka kumsaini mchezaji nyota wa Colombia James Rodriguez,27,ambaye anatarajiwa kuondoka Bayern Munich mkataba wake wa mkopo utakapokamilika msimu huu. (Mirror)

Rais wa Bayern Munich president Uli Hoeness amethibitisha kuwa mabingwa hao wa Bundesliga wanamtaka winga wa Manchester City Mjerumani Leroy Sane. (Suddeutsche Zeitung – in German)

City wanajiandaa kuweka dau la kumnunua nyota huyo wa miaka 23 kutoka kwa miamba hao wa ujerumani ambalo linatarajiwa kuvunja rekodi. (Mail)

Arsenal wanataka kumsaini winga Ryan Fraser, 25, baada ya fainali ya ligi ya Europa, lakini Bournemouth wanataka kulipwa £30m kumwachilia kiungo huyo wa kimataifa wa Uskochi. (Independent)

Tottenham wamewasiliana na Real Madrid ili kuanza mazungumzo ya kutaka kumnunua kiungo wa kati Marco Asensio, 23, lakini wameambiwa mchezaji huyo rai wa Uhispania hapatikani. (AS – in Spanish)

Marco AsensioHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image caption Marco Asensio (Kulia)
Kocha wa Newcastle Rafael Benitez amewambia Marseille na Roma kuwa kipaumbele chake ni kukubali mkataba mpya St James Park baada ya wao ku kuonesha ari ya kutaka kumpatia kazi ya umeneja. (Chronicle)
Wachezaji Matteo Darmian, 29, Romelu Lukaku 26, Juan Mata, 31, na Marcos Rojo – huenda wakondoka Manchester United msimu huu(Mirror)

Inter Milan itatangaza ofa ya zaidi ya £30m winga wa Croatia winger Ivan Perisic, 30, ili kumnunua Lukaku. (Gazzetta dello Sport – in Italian)

Ivan PerisicHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image caption Ivan Perisic
Manchester City wanataka £15m kumuuza kiungo wa kati Fabian Delph, huku vilabu kadhaa vya ligi ya Premier vikimnyatia nyota huyo wa miaka 29. (Sun)
Mshambuliaji wa Crystal Palace sChristian Benteke, 28, huenda akaondoka Selhurst Park msimu huu baada ya kukubali dau la £15m la kumnuuza nyota huyo wa kimataifa wa Ubelgiji kutoka klabu ya China ya Shandong Luneng Taishan. (Times – subscription required)
Christian BentekeHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image caption Christian Benteke(Kulia)
Napoli wanatarajiwa kumsaini beki wa kulia- kushoto wa Tottenham Kieran Trippier, 28, huku Mwingereza huyo akipewa idhini ya kukubali ofa nzuri. (Independent)
Manchester United wanatarajiwa kumsaini mshambuliaji mshambuliaji Dillon Hoogewerf baada ya kucheza mechi ua vijana wa Ajax. (Metro)

Arsenal ni moja ya vilabu vinavyofuatilia mchezo wa mshambuliaji Danny Loader, 18 raia wa Ungereza. (Goal)

Brendan RodgersHaki miliki ya pichaSNS

Image caption Kocha wa Leicester, Brendan Rodgers (Kulia)
Meneja wa Leicester Brendan Rodgers anatathmini uwezekano wa kuungana tena na winga Patrick Roberts, ambaye alicheza chini yake wakati alipokua Celtic. (Sun)

Leave a comment