Sherehe za Ubingwa Simba Kufanyika Leo

Mabingwa wa nchi Simba leo wanakabidhiwa taji la pili mfululizo ligi kuu ya Tanzania Bara baada ya mchezo dhidi ya Biashara United

Mchezo huo utaanza mapema tu, saa tisa Alasiri ambapo hafla ya makabidhiano ya ubingwa itafanyika baada ya mchezo huo

Waziri wa Mambo ya Ndani Mh Kangi Lugola anatarajiwa kuwa mgeni wa rasmi katika hafla hiyo itakayofanyika uwanja wa Taifa

Uongozi wa Simba umewataka mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi uwanja wa Taifa leo kushuhudia tukio hilo litakalobaki kwenye kumbukumbu za klabu ya Simba

Hilo ni taji la 20 la ligi kuu ya Tanzania Bara kwa Simba

Baada ya kuichachafya Sevilla juzi, Aussems amepania kushusha mziki kamili ili kunogesha sherehe za ubingwa kwa ushindi mnono

Viingilio vya mchezo huo, VIP A Tsh 15,000/- VIP B na C Tsh 10,000/- wakati mzunguuko ni Tsh 3,000/-