ADAM SALAMBA: Kuweka Kumbukumbu kiatu cha Banega

Baada ya mchezo wa Kimataifa wa kirafiki dhidi ya Sevilla, tukio la mshambuliaji wa Simba Adam Salamba kumuomba kiatu kiungo mahiri na nahodha wa Sevilla Ever Banega, liliibua mijadala kwenye mitandao ya kijamii

Baadhi ya mashabiki hawakuelewa maana ya tukio hilo ambalo ni la kawaida na hufanywa na wanasoka kama sehemu ya kuonyesha uungwana mchezoni

Salamba amesema ataweka kumbukumbu kiatu alichopewa na kiungo huyo wa Kimataifa wa Argentina

“Kiatu ambacho nimepewa na mchezaji wa kimataifa kutoka Sevilla, Ever Banega nitakichongea fremu iwe kumbukumbu daima,” amesema

Aidha Salamba amesema fursa ya kucheza na Sevilla imemuongezea shauku ya kutaka kwenda kucheza soka nje ya nchi

“Ndoto zangu ni kucheza nje ya Tanzania, baada ya kucheza na Sevilla juzi, imeniongezea ari ya kutaka kufikia malengo hayo”