Francis Kahata amegoma kuongeza mkataba katika klabu hiyo huku akihusishwa kusajiliwa na Simba mkataba wake utakapomalizika mwezi wa saba

Kiungo fundi wa Gor Mahia Francis Kahata amegoma kuongeza mkataba katika klabu hiyo huku akihusishwa kusajiliwa na Simba mkataba wake utakapomalizika mwezi wa saba

Msimu huu Kahata ameisaidia Gor Mahia kutwaa taji la ligi kuu ya Kenya pamoja na kuisaidia timu hiyo kufika hatua ya robo fainali kombe la Shirikisho Barani Afrika

Hata hivyo fundi huyo wa mpira anataka kuungana na Meddie Kagere mshambuliaji wa zamani wa Gor Mahia ambaye kwa sasa yuko Simba

Inaelezwa Kagere amemshawishi kiungo huyo ambaye walicheza nae katika klabu ya Gor Mahia

Gor Mahia inakabiliwa na hali ngumu ya kiuchumi na huenda ikawapoteza nyota wake muhimu wanaowania na timu kadhaa

Mshambuliaji tegemeo wa timu hiyo Jacques Tuyisenge yuko mbioni kukamilisha usajili kunako klabu ya Atletico De Luanda ya nchini Msumbiji

Baada ya kumkosa msimu uliopita, Simba ina nafasi nzuri ya kumsajili Kahata msimu huu