Jana mashabiki wa Simba waliojitokeza uwanja wa Taifa kushuhudia ‘mnyama’ akikabidhiwa kombe baada ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu, hawakufurahia kuahirishwa kwa hafla hiyo
Licha ya mvua kunyesha, baadhi ya mashabiki walikubali ‘kulowana’ ili mradi tu washuhudie tukio hilo la kihistoria
Hata hivyo Bodi ya ligi iliahirisha hafla hiyo baada ya mgeni rasmi, Waziri wa Mambo ya Ndani Mh Kangi Lugola kupata udhuru
Mtendaji wa Bodi ya Ligi Boniface Wambura alisema sherehe hizo zimehamishiwa mkoani Morogoro, zitafanyika baada ya mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar utakaopigwa keshokutwa Jumanne katika uwanja wa Jamhuri
Akingumza baada ya mchezo dhidi ya Biashara United uliomalizika kwa sare ya bao 1-1, nahodha wa Simba John Bocco aliwashukuru mashabiki waliojitokeza uwanja wa Taifa kuwaunga mkono licha ya hali ya mvua