Barcelona yamuachia kiungo wao denis Suarez

credit: @sokawaytz_…

✍🏻 Dili la Uhamisho wa kiungo wa Mhispania, Denis Suarez “25” kutoka FC Barcelona kwenda Celta Vigo limetimia na Vilabu vyote Vimethibitisha kufikikia Makubaliano; Sasa ni Official Kiungo huyo kasaini Miaka Minne kukipiga Celta Vigo huku Akisajiliwa kwa dau La Uhamisho €15m.. Hivyo Suarez anarejea alipoanzia Maisha ya Soka.

.

– Suarez alicheza Celta B mwaka 2010, Baada ya hapo Akasajiliwa Manchester City. Akadumu Misimu miwili tu England bila kupata nafasi timu ya kwanza. Akaamia La Masia Academy ya FC Barcelona mwaka 2013. Baada ya msimu akatolewa kwa mkopo kwenda Sevilla ya Unai Emery akacheza games 31 hapo. Akauzwa kwenda Villareal Kipengele cha Barça kumnunua wao na wakamnunua kweli baada ya misimu miwili..

.

– January 2019 akatolewa kwa mkopo kwanda Arsenal akiungana na kocha Unai Emery tena, Hapo London alicheza mechi Nne tu mpaka msimu ulipofikia mwisho majeraha hasa yalimuweka nje na hatimae Sasa kauzwa..

#LaligaTransferUpdates

@sokawaytz_

Leave a comment