Yanga yajitapa kufanya maajabu msimu ujao

credit: @simbamakini…

YANGA YAAHIDI KUFANYA MAAJABU AFRIKA

Uongozi wa klabu ya Yanga umejinasibu kufanya vizuri katika michuano ya klabu bingwa Afrika (CAF) msimu ujao kuliko ilivyowahi kufanya misimu iliyopita.

Yanga tayari imetuma CAF majina 26 ya wachezaji jana ambayo imewasajili kwa ajili ya michuano hiyo.

Kaimu Katibu mkuu wa klabu hiyo, Dismas Ten amesema kwa wachezaji waliowasajili msimu huu wana matumaini ya kufanya makubwa katika michuano hiyo ya CAF pamoja na ligi ya nyumbani. “Jana tumetuma majina 26, CAF ya wachezaji ambao tumewasajili msimu huu, matumaini yetu ya kufanya vizuri ni makubwa sana,” alisema Ten.

Leave a comment