Man united atashinda leo thidi ya Chelsea

credit: @sokawaytz…

🔙🔙 August 11; Siku kama ya leo Mwaka 2013, Manchester United iliitwanga Wigan 2-0 Katika fainali ya FA Community Shield “Ngao ya Jamii”. Hii ilikuwa Ni game ya kwanza ya Kocha David Moyes ndani ya United, na Kwa Mara ya kwanza kwa The Red Devils kucheza mechi bila ya kuwepo Katika Benchi Aliyekuwa Kocha Mkuu, Sir Alex Ferguson tangu November 1986.

.

– Manchester United walikuwa Mabingwa wa Premier league Mwaka uliopita, na Wigan walikuwa Mabingwa wa FA Cup Mwaka uliopita, Wigan walicheza fainal hiyo wakiwa wameshuka Daraja, ndio ilikuwa timu ya kwanza kutoka nje ya Premier league kucheza mechi ya Ngao ya Jamii tangu Mara ya mwisho wacheze West Ham United 1980!.

.

– Kwa Mwaka huo, United iliweka Rekodi ya kutwaa Mara nyingi zaidi Ngao hiyo ikiwa Ni ya 16 Kipindi hicho… Man of the Match alikuwa Ni Michael Carrick na mwamuzi wa Mchezo Ni Mark Clattenburg ndani ya Wembley Stadium huko London uwanja ulijaa kwa Watazamaji, 80,235..

:

Leave a comment