Wanachama wa klabu ya Yanga wamemtaka Mwenyekiti wa klabu hiyo Yusufu Manji ajitokeze hadharani kumaliza utata baada ya Baraza la Michezo (BMT) kuitaka klabu hiyo ijaze nafasi yake.
Jana Wanachama wa Yanga kupitia viongozi wa Matawi walimtaka Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini Mzee George Mkuchika kuitisha Mkutano Mkuu wa dharura ili kumaliza utata wa sakata la Manji
Katibu wa Matawi hayo Boaz Ikupilika alisema kwa kuwa wanachama wa Yanga ndio waliomchagua Manji na baadae kuikataa barua yake ya kujiuzulu, basi ni vyema ukaitishwa Mkutano huo ambao Manji ataalikwa ili kuwaeleza wanachama waziwazi kama amejitoa kwenye uongozi wa Yanga ili wafanye uchaguzi kama ilivyoagizwa na BMT
Yanga imepewa mwezi mmoja kuhakikisha imefanya uchaguzi.
Hata hivyo kumetokea mvutano baina ya wanachama wa klabu hiyo ambapo wengine wametaka kufanyika kwa uchaguzi kama ilivyoagizwa na BMT huku wengine wakipinga uchaguzi kwa kuwa bado wanamtambua Manji kuwa Mwenyekiti wa Yanga