Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amekerwa na ubutu wa safu yake ya ushambuliaji baada ya timu yake kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Ndanda Fc kwenye mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara uliopigwa jana usiku.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mchezo ya mchezo jana, Zahera alisema timu yake ingeweza kuondoka na ushindi mnono kama wangetumia vyema nafasi walizotengeneza.
“Jana tulicheza sana mpira tofauti na michezo mingine. Tulitengeneza nafasi nyingi sana ambazo hatukuzitumia,”amesema
Zahera amemshukia mshambuliaji Heritier Makambo aliyekosa nafasi kadhaa za wazi
“Kila mechi tunatengeneza nafasi nyingi lakini washambuliaji hawafungi. Mfano goli la kichwa alilokosa Makambo hata Mama yangu angeweza kufunga,” alisema aliyeonekana kukerwa na hali hiyo.