Beki kisiki wa Simba, Paschal Wawa amempa jeuri kocha Mkuu Patrick Aussems ya kutokuwa na presha ya kusajili mabeki kwenye usajili wa dirisha dogo kwa kuwa anafanya kazi yeke ipasavyo.
Aussems amesema kuwa kwa sasa hafikirii kuongeza beki wa kati ndani ya kikosi chake kwa kuwa wale waliopo wanatosha na wanafanya kile ambacho anawaelekeza hali inyompa amani.
“Nafasi ya beki wa kati sifikiri kama nitaongeza mchezaji . Hawa waliopo wakiongozwa na Wawa ni wazuri na wanaonyesha uwezo mkubwa katika mechi zetu wanazocheza,” Aussems amenukuliwa na GPL
Mabeki wa kati wa Simba Erasto Nyoni, Juuko Murshid na Paul Bukaba wameonyesha viwangi vizuri katika michezo waliyocheza kwani wameruhusu mabao manne tu katika mechi 11 za ligi.
Pia yupo beki chipukizi Yusufu Mlipili ambaye licha ya kutopata namba msimu huu, anaweza kuisaidia Simba pale atakapohitajika na kocha Aussems