Tanzania Prisons ipo kwenye mikakati ya kuimarisha safu yake ya ushambuliaji katika kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili.
:
Katibu wa timu hiyo Havinitishi Abdallah amesema miongoni mwa wachezaji wanaowataka ni pamoja na mshambuliaji wao wa zamani Mohamed Rashid ambaye kwa sasa yupo Simba.
:
“Tunajipanga kwenye dirisha dogo ili kufanya vizuri kwa sababu ukiangalia tatizo lipo kwenye ushbuliaji ndio tunataka kuongezea kwenye maeneo hayo kwa hiyo baada ya siku mbili tatu tutasema kitu kwa sababu tayari tumeanza mazungumzo na vilabu kutupa wachezaji kwa mkopo.
:
“Kuna wachezaji wapo Azam mwingine ni Mohamed Rashid yupo Simba, hivyo tunasubiri ndugu zetu watujibu na taarifa tumeshapeleka kuwaomba kwa mkopo.”
:
“Timu yetu siyo mbaya, inacheza vizuri na kutengeneza sana nafasi tatizo lipo kwenye kufunga na ndio tunalifanyia kazi. Sehemu nyingine zipo sawa.”