Imebainika kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera ndiye aliyependekeza kusajiliwa kwa kiungo wa African Lyon, Haruna Moshi ‘Boban’.
Tayari Yanga imeshamalizana na Boban ambaye amesaini mkataba wa miezi sita.
Zahera amebainisha kuvutiwa na Boban alipomuona kwenye mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara kati ya African Lyon dhidi ya JKT Tanzania
Baada ya kuvutiwa na uwezo wake, Mcongomani huyo aliwaagiza viongozi wa Yanga kumfuatilia na kukamilisha usajili wake.
Boban ana uzoefu wa soka la Tanzania, na ni miongoni mwa wachezaji walion’gara kwenye kikosi cha African Lyon msimu huu.
