Kagere, Chama hawaendi kokote – Mo

Mwekezaji wa klabu ya Simba Mohammed Dewji ‘Mo’ amesema wachezaji Meddie Kagere na Clatous Chama wataendelea kubaki Msimbazi kwa kuwa timu hiyo inawahitaji kufikia malengo yake ya kupata mafanikio makubwa kwenye soka la Afrika

Simba inadaiwa kuwa na ofa nyingi mezani kutoka kwa vilabu vikubwa barani Afrika kutaka huduma za wachezaji hao ambao wamekuwa chachu ya mafanikio ya kikosi cha Simba hasa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika msimu huu

“Simba bado tunajenga timu, Meddie Kagere na Clatous Chama bado wanamikataba, ni kweli Simba tunahitaji pesa lakini tunahitaji ushindi na mafanikio kuliko pesa,” amesema Mo

“Kwa mwaka huu bonus tutakazotoa kwa wachezaji zitafika zaidi ya Billion 1. Mara nyingi unaweza kuona tumejaza uwanja lakini asilimia kubwa ya hizo pesa zinakwenda kwenye bonus za wachezaji kama tungefikiria pesa zaidi hizo bonus tungeshusha lakini sisi tunataka tuwape ari zaidi wachezaji wetu ili tupate mafanikio zaidi.”

“Kwa hiyo kwa hao wachezaji wawili mimi sio kocha lakini naimani kocha atataka kuendelea nao, kwa hiyo itakuwa ngumu kuwatoa Simba labda iwe kwa bei kubwa sana ili sisi tuweze kupata wachezaji wengine, hiyo itakuwa ni habari nyingine.”