
Kinara huyo wa kutengeneza mabao ligi kuu huenda akarejea kikosini kwenye mchezo ujao dhidi ya Mtibwa Sugar utakaopigwa mkoani Morogoro April 17 2019
Kukosekana kwake katika michezo iliyopita kumeibua maswali mengi miongoni mwa mashabiki wa Yanga hasa baada ya kuibuka tetesi kuwa anataka kurudi katika timu yake ya zamani, Simba
Hata hivyo Msemaji wa Yanga Dismas Ten amesisitiza kuwa Ajib amekosa michezo iliyopita kutokana na kuwa majeruhi na si vinginevyo
Amesema atarejea kikosini baada ya kupona majeraha hayo