Mchezo kati ya Coastal Union dhidi Simba Sc uliotakiwa kuchezwa kesho majira ya saa 10:00 Jioni katika uwanja wa Mkwakwani Tanga, umerudishwa nyuma kwa masaa mawili na sasa utapigwa majira ya saa nane mchana. .
.
Maamuzi hayo yametolewa na shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF ili kuipa nafasi michuano ya vijana AFCON U17 inayoendelea jijini Dar Es Salaam
TAARIFA MUHIMU. .
Mratibu wa klabu ya Yanga Sc Hafidh Saleh amethibitisha kuwa mchezo wao wa kesho dhidi ya Mtibwa Sugar uliotakiwa kupigwa majira ya saa 10 Jioni umerudishwa nyuma kwa masaa mawili na sasa utapigwa majira ya saa 8:00 mchana. .
.
Mchezo huo umerudishwa nyuma ili kupisha mchezo wa AFCON U17 kati ya Serengeti Boys dhidi ya Uganda utakaopigwa majira ya saa 10 Jioni