Tshishimbi aumia mazoezini

Kiungo Mcongoman Papi Tshishimbi amepata majeraha katika mazoezi ya Yanga leo asubuhi uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro hivyo kumuweka kwenye hatihati ya kukosa mchezo wa kesho

Tshishimbi ameuamia enka, hatma ya kama kesho ataweza kucheza au la itategemea ripoti ya Daktari wa Yanga Dk Edward Bavu

Yanga itachuana na Mtibwa Sugar kesho Jumatano katika mchezo wa ligi kuu ambao utapigwa saa nane mchana kwenye uwanja wa Jamhuri