FT : Kagera Sugar 2-1 Simba

Mabingwa watetezi ligi kuu ya Tanzania Bara Simba leo wamepoteza mchezo wa pili msimu huu baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Kagera Sugar

Kagera Sugar ilikuwa bora zaidi kwenye kipindi cha kwanza ambapo ilipachika mabao yake mawili yaliyofungwa na Kassim Khamis na Ramadhani Kapera

Simba ilikuja juu kwenye kipindi cha pili na kufanikiwa kufunga bao lake kupitia kwa Emmanuel Okwi kwenye dakika ya 64

Wekundu wa Msimbazi walikosa nafasi kadhaa ambazo zingewawezesha kuondoka na angalau alama moja dhidi ya Kagera Sugar ambayo kwa mara nyingine imedhihirisha umwamba wake dhidi ya Simba

Simba haikuwa katika kiwango bora leo, pengine uchovu uliosababishwa na timu kucheza mfululizo umechangia kukosa matokeo muhimu

Baada ya mchezo huo Simba inaelekea mkoani Mwanza ambapo Jumanne, April 23 itacheza na Alliance Fc