
Kutokana na umuhimu wa Kila Mwanayanga ambae anatoa pesa yake kwa ajili ya timu yetu TUIPENDAYO na yenye Thamani kubwa sana kwetu sote, Kamati imefikia uamuzi ufuatao ili kujenga wigo mpana wa kila mtu kuwa sehemu ya tukio hili muhimu linalohusu uchangiaji wa Klabu yetu.
Tukio Maalum la chakula cha jioni jijini Dar es salaam litafanyika siku ya Jumamosi tarehe 11/05/2019 Hotel ya Serena kuanzia saa kumi na mbili jioni.
Makundi ambayo yatakuwa yameshachangia shilingi milioni moja au zaidi yatapewa kadi ya mualiko na kumteua mtu mmoja ambaye ataliwakilisha kwa niaba na hatimaye aweze kushiriki kwenye Chakula Cha Jioni pamoja na kupokea CHETI MAALUMU cha Shukurani kwa niaba ya kundi lake.
Kamati imeona ni busara kupata uwakilishi huo wa mtu mmoja mmoja kutokana na eneo husika kubeba idadi isiyozidi watu mia tano.
Kwa mantiki hiyo tunaamini tutakuwa tumeweza kushirikisha kila kundi au mtu kwenye matukio haya muhimu kwa Klabu yetu.
TUENDELEE KUICHANGIA TIMU YETU ILI TUWE NA KIKOSI SHINDANI MSIMU UJAO
Timu ya Wananchi Wawekezaji ni Wananchi
Deo Mutta
KATIBU – KAMATI YA HAMASA
YANGA 23/04/2019