Yanga yajitathmini faini za kila mara

Uongozi wa Yanga umesema utachukua hatua ili ‘kujisahihisha’ kuepuka faini za Shirikisho la Soka nchini (TFF) kutokana na matukio yanayohusisha imani za kishirikina yanayojiri kwenye baadhi ya michezo yake

Matukio ya kutotumia mlango rasmi wa kuingia uwanjani yameigharimu sana Yanga msimu huu ambapo jana ilipigwa faini ya nne baada ya kufanya kosa hilo mkoani Mtwara ilipokwenda kucheza na Ndanda Fc

Yanga tayari imepigwa faini zilizoigharimu timu hiyo zaidi ya Tsh Milioni 10 kutokana na matukio hayo ya kuingia uwanjani kwa kutumia ‘njia za panya’

Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten amesema matukio hayo yanachangiwa zaidi ya Wananchi ambao kimsingi ndio wenye timu na wanahusishwa kuisimamia timu inapokwenda kucheza

“Umefika wakati sasa tunapaswa kuwaelimisha watu wetu wafahamu athari tunazopata kutokana na kuendekeza imani hizi,” amesema

“Lazima ifahamike kila mchezo una kanuni na taratibu zake. Tukiendelea kuvunja kanuni kutokana na imani zetu, tutaendelea kuigharimu timu”