Majanga ya msimu uliopita yaikumba tena Yanga

Wakati kikosi cha Yanga kikitarajiwa kuchuana na Azam Fc Jumatatu, April 29 katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara, kocha Mwinyi Zahera huenda akalazimika kutumia wachezaji wa kikosi cha pili kufuatia mgomo unaofanywa na wachezaji wa kikosi cha kwanza

Leo Zahera aliamua kutumia wachezaji wa Yanga B kujiandaa na mchezo dhidi ya Azam FC baada ya wachezaji wa kikosi cha kwanza kugoma tena kufanya mazoezi licha ya kufika mapema uwanja wa chuo cha Polisi Kurasini

Mwishoni mwa msimu uliopita Yanga ilikumbana na changamoto kama hii ya wachezaji kugoma wakishinikiza walipwe hali iliyopelekea kumalizia michezo ya mikaoni ikiwa na kikosi cha wachezaji 14

Huenda hali hiyo ikajirudia tena kwa michezo sita iliyobaki kama viongozi wa muda wa Yanga hawatachukua hatua za haraka kutatua mgogoro uliopo