Manara awapasha Yanga, ‘kalipeni mishahara ya wachezaji wenu’

Afisa Habari wa Simba Haji Manara amewataka mashabiki wa Yanga watumie muda wao kuinusuru timu yao na ‘ukata’ uliowakumba kuliko kupoteza muda mwingi kuifuatilia Simba ambayo inafanikiwa mambo yake

Baada ya mchezo dhidi ya KMC jana, mashabiki wa Yanga walionekana kuisemea KMC kuwa imeonewa na waamuzi huku wachezaji wa timu yao wakigoma kufanya mazoezi wakidai mishahara

Tangu jana wachezaji wa Yanga hawafanyi mazoezi wakishinikiza walipwe madai yao ya mishahara ya miezi mitatu huku wengine wakiwa hawajalipwa fedha za usajili mpaka leo

“Badala ya kuhangaika jinsi ya kuwalipa mishahara wachezaji wenu mnahangaika na timu Bingwa inayowafunga kila siku. Kama nyie wananchi wachangieni hao wachezaji walipwe mishahara,” ameandika Manara kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram