Mchezo wa Biashara United vs Simba utapigwa hapa

Simba kesho Jumamosi itandelea na ratiba yake ya ‘bandika-bandua’ kwa kuikabili Biashara United katika mchezo utakaopigwa dimba la Karume wilayani Musoma

Simba tayari imeondoka Mwanza na leo jioni inatarajiwa kujifua kwenye uwanja huo

Hii itakuwa mara ya kwanza kwa Simba kucheza mkoani Mara baada ya kupita miaka 15

Biashara United inanolewa na beki wa zamani wa Simba Amri Said