Timu ya Sevilla imewasili nchini usiku wa kuamkia leo tayari kwa mchezo wa Kimataifa wa kirafiki dhidi ya Simba utakaopigwa kesho Alhamisi, saa moja jioni katika uwanja wa Taifa
Katika Mkutano na Waandishi wa habari leo, Rais wa Sevilla Jose Castro ameeleza kufurahia ujio wao hapa nchini hasa ikizingatiwa wao wanakuwa timu ya kwanza kutoka Hispania kucheza Tanzania
Aidha ameipongeza Simba kwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Tanzania Bara
“Niwapongeze sana Simba ya Tanzania kwa kuchukua ubingwa wa ligi Kuu, tumekuja kucheza na timu bora. Ni heshima sana kuja Tanzania na bila shaka tutakua ni timu ya kwanza ya Laliga kuja Tanzania,” amesema
Wakati Sevilla ikiwa tayari imewasili, wapinzani wao Simba nao watatua leo kutoka mkoani Dodoma baada ya kufanikiwa kutetea ubingwa wa ligi kuu kwa msimu wa pili mfululizo