YANGA DIMBANI LEO KUIVAA MBEYA CITY

Kikosi cha Yanga leo kinashuka uwanja wa Uhuru kuikabili Mbeya City katika mchezo wa ligi kuu raundi ya 37

Baada ya Simba kutwaa ubingwa hapo jana, mchezo huo ni wa kukamilisha ratiba tu ambapo mabingwa hao wa kihistoria watakuwa wakilinda heshima yao

Jana Yanga ilifanya maandalizi ya mwisho kwenye uwanja wa Uhuru
Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema lengo lao ni kumaliza ligi kwa kushinda michezo yote miwili iliyobaki
Ushindi katika michezo miwili iliyobaki utawafanya wafikishe alama 89 ambazo hata hivyo tayari zimeshapitwa na Simba yenye alama 91

Lakini pia hata kama Yanga itapoteza michezo yote iliyobaki, itaendelea kubaki nafasi ya pili kwani hakuna timu nyingine inayoweza kufikisha alama hizo
Yanga leo inatarajiwa kuwakosa wachezaji saba ambao wanaugua Malaria

Hata hivyo Zahera amesema wachezaji watakaopata nafasi ya kucheza, anaamini wataweza kuipa timu hiyo ushindi
Baada ya mchezo wa leo, Yanga itashuka tena dimbani wiki ijayo May 28 kumaliza msimu kwa kuumana na Azam FC

Leave a comment