FT: Simba 1-1 Biashara United

Mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara kati ya Simba, mabingwa msimu huu na Biashara United umemalizika kwa timu hizo kutoka sare ya kufungana bao 1-1

Mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa Taifa, ulivurugwa na mvua zilizojaza maji katika sehemu ya kuchezea ya dimba la Mkapa

Biashara United ilitangulia kupata bao la kuongoza kupitia kwa Innocent Edwin kwenye dakika ya 14 na Simba ikasawazisha dakika tatu baadae kupitia kwa Clatous Chama

Mashabiki hawakujitokeza kwa wingi uwanjani kutokana na hali ya mvua inayoendelea kunyesha jijini Dar es salaam

Yatibua sherehe za ubingwa

Bodi ya Ligi imelazimika kuahirisha sherehe za kuwakabidhi Simba kombe kutokana na changamoto ya mvua

Aidha Mtendaji wa Bodi Boniface Wambura amesema mgeni Rasmi Mh Kangi Lugola naye alipata dharura

Simba sasa itakabidhiwa ubingwa mkoani Morogoro siku ya Jumanne, itakapochuana na Mtibwa Sugar katika mchezo wa kumaliza msimu

Uongozi wa Simba umewataka mashabiki wa timu hiyo mkoani Morogoro kujiandaa kuipokea timu na kuwa tayari kwa shamrashamra za kihistoria