YONDANI: Amtibua ZAHERA

Kikosi cha Yanga leo kimeendelea na mazoezi kwenye uwanja wa Chuo cha Polisi Kurasini jijini Dar es salaam kujiandaa na mchezo wa mwisho wa ligi kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Azam Fc utakaopigwa Jumanne, May 28 dimba la Uhuru

Kocha Mkuu wa mabingwa hao wa kihistoria Mwinyi Zahera amesema baadhi ya wachezaji waliokuwa wagonjwa wameanza kurejea kikosini

“Paul Godfrey alikuwa mgonjwa lakini leo ameanza mazoezi. Dante, Abdul, Ngasa, Banka, Jaffar na Ajib bado wagonjwa,” amesema

Katika hatua nyingine Zahera amemuagiza Meneja wa Yanga Nadir Haroub kumsaka beki wa timu hiyo Kelvin Yondani ambaye haonekani mazoezini

Zahera amesema hana taarifa kama Yondani ni mgonjwa, amejaribu kumpigia simu bila ya mafanikio

“Sina taarifa za Yondani, nimejaribu kumpigia simu lakini hapokei, tumemtuma Meneja (Nadir) aende akamtafute kwake anipe mrejesho kabla sijafanya maamuzi,” Zahera aliiambia eFM