Stock city yamtema mshambuliaji wa Burundi saida Beraino

– Klabu ya Stoke City Inayoshiriki Championship nchini England, Imethibitisha kusitisha Mkataba na Mshambuliaji wake, Saido Berahino; Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25 ambaye alikutwa na kosa La Ulevi akiwa anaendesha gari mwezi huu na kufungiwa kuendesha vyombo vya Moto Uingereza, na kupigwa faini ya £75,000 na Mahakama ya Highbury Corner Magistrates.

:

– Mnamo Januari 2017, Berahino alijiunga na Stoke kutokea West Bromwich Albion kwa ada ya uhamisho £12m na alisaini Mkataba wa miaka Mitano, Amecheza michezo 51 ya ligi akifunga magoli matatu; Tangu akutwe na Makosa ya Ulevi hajawahi tena kupangwa katika kikosi cha timu yake mpaka walipotoa taarifa ya kuvunja Mkataba uliokuwa umalizike 2022.

:

– Mwezi ujao, Berahino atatarajiwa kuwa sehemu ya Kikosi cha Burundi katika Mechi za Mataifa ya Afrika AFCON 2019 nchini Misri..Vijana hao wa kocha Olivier Niyungeko wamepangwa kundi B, ambapo watacheza na Nigeria Juni 22 kabla ya kucheza Madagascar siku tano baadaye na kumaliza na Guinea siku ya Juni 30..

#Updates

@Sokawaytz

credit: @sokawaytz

Leave a comment