
– Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB), ameitangaza timu ya Stand United ya Shinyanga kushuka daraja moja kwa moja badala ya Kagera Sugar kama ilivyotangazwa jana kwenye msimamo wa Shirikisho la soka Nchini Tanzania (TFF).
.
– Ofisa Mtendaji Mkuu wa TPLB, Boniface Wambura Mgoyo, amewaambia Waandishi wa Habari Mchana huu Jijini Dar Es Salaam kwamba, kulikuwa na makosa katika uingizwaji wa matokeo ya mechi moja iliyowakutanisha Kagera Sugar na Stand United ambapo badala ya kuingiza Stand wameshinda 3-1, watu wa Data wa Bodi ya Ligi wakaingiza kimakosa 3-0, hivyo kuharibu uwiano wa jumla wa magoli ya kufunga na kufungwa baina ya timu hizo.
.
– Wambura amewaomba radhi wadau wa soka kwa kosa lililojitokeza na kusema Ofisi yake inawajibika kwa kumpa adhabu Ofisa aliyepotosha takwimu; RASMI: Kagera Sugar wanarejea kucheza Playoff dhidi ya Pamba SC, na Mwadui FC watakabiliana na Geita Gold SC… Game za kwanza za Playoffs kupigwa Juni 02 na Game za Marudiano kupigwa Juni 08 mwaka huu.
#Updates
@Sokawaytz
credit: @sokawaytz
