
credit: @sokawaytz…
✍🏻 Klabu ya Yanga SC Imeendeleza vurugu zao kwenye suala zima la usajili baada ya kushusha beki mwingine wa Kimataifa wa Burundi, Moustafa Selemani; Moustafa ametua jana akitokea kwao Burundi katika Klabu ya Aigle Noir FC Ambao pia ndio Mabingwa wa Burundi msimu huu.
:
✍🏻 Beki huyo ambaye Pia ni Nahodha wa Timu ya taifa ya Burundi U23, kabakiza mwezi tu katika Mkataba wake na Aigle Noir, na kwa mujibu wa Taarifa ni tu ni kwamba kafikia Makubaliano ya Kusaini Mkataba wa Miaka miwili na Mabingwa wa Kihistoria Tanzania Klabu ya Yanga SC.. Nyota huyo Sasa ni beki wa Pili wa Kimataifa kusinyaa Jangwani Baada ya Mghana, Lamine Moro kumwaga wino siku chache zilizopita..
#transfers #updates
@Sokawaytz