Stars yaanza na Senegal Afcon

credit: @sokawaytz…

– Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania, Emmanuel Amunike, amesema kuwa anaamini kuwa kushinda mechi ya ufunguzi katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika “AFCON” zitasababisha mafanikio kwenye Mashindano hayo kwani kutakuwa na nguvu ya kushinda mechi zinazofuata.

.

– Taifa Stars Imepangwa kuanza na Senegal katika Mchezo wa kwanza wa Kundi la C na legend huyo wa Nigeria anaamini matokeo ya ushindu yataamua muendelezo wa timu katika mashindano huko Misri.

:

🗣 “Tutafungua kampeni yetu ya AFCON dhidi ya Senegal. Kwangu mimi, Senegal ni timu bora Afrika hadi sasa ina wachezaji wengi wazuri, lakini bado tuna wachezaji wetu wazuri ambao wanaweza kuleta matokeo yaliyoridhisha”.

.

🗣 “Unapoingia katika mashindano haya, unapaswa kupata matokeo mazuri ya kwanza ili upate na hakika ya kufanya vizuri na hivyo ndio tutakavyolenga dhidi ya Senegal, kushinda mechi yako ya kwanza katika Mashindano yoyote husaidia sana kuimarisha timu mbele ya mechi nyingine zinazokuja” Amunike aliwaambia Waandishi wa Habari kambini jijini Aleksandria..

#Updates

@Sokawaytz

Leave a comment