
credit: @sokawaytz_…
– Aliyekuwa Kiungo Mshambuliaji wa Klabu ya Yanga SC, Ibrahim Ajibu amewashukuru Mashabiki na Viongozi na Benchi la Ufundi la Klabu hiyo Baada ya kukamilisha usajili wake wa kujiunga na Watani zao, @simbasctanzania, Ajibu ameandika katika Mtandao wake wa kijamii wa Instagram.
:
##Repost
Hakika Ilikua miaka miwili bora sana kwangu, ndani na nje ya uwanja, Yanga ilikua sehemu ya familia yangu.
Nitoe shukrani zangu za dhati kwa viongozi, benchi la ufundi, wachezaji na mashabiki wote, kwa kuniamini na kuniunga mkono katika kila jambo.
Ni mengi nimejifunza na nina amini yatanisaidia kunijenga zaidi kama mchezaji. Asanteni sana.
Hadi wakati mwingine tena, Wananchi🙏🏻